Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, 4 February 2014

Sunday, 26 January 2014

Mwaka 2014 uwe wa waandishi kujirekebisha



Mwaka huu wa 2014, uwe ni mwaka wa kujirekebisha katika uandishi kwani yako matukio mengi ya kihistoria yatakayotokea.
Matukio haya ni maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao, kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya, utayarishaji wa Rasimu ya Katiba ya Tanganyika, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mambo kama hayo.

Msekwa, Kisumo wakoleza moto


 Pius Msekwa>PICHA MAKTABA 
Dar es Salaam. Wakati mjadala wa uteuzi wa mawaziri ukiendelea kupamba moto nchini, makada wakongwe wa CCM, Pius Msekwa na Peter Kisumo wamesema Rais Jakaya Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteua na habanwi na chama, wala mtu yeyote.

Saturday, 25 January 2014

Operesheni ya ujangili yaundiwa mahakama sasa


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema mchakato wa kuwapata wajumbe wa Tume ya Kimahakama ya Kuchunguza Madhara ya Operesheni Tokomeza Ujangili umeshaanza na majina hayo yatawekwa wazi hivi karibuni.

Mvua yaharibu miundombinu reli


Nyumba ikiwa imeharibiawa na mvua iliyoambatana na upepo mkali mkoani Dodona. Mpigapicha wetu 
Dar es Salaam. Wakati timu ya wahandisi ikiendelea kufanya tathimni na marekebisho ya awali ya kipande cha reli reli kilichoharibika eneo la Godegode kutokana na mvua kubwa zilizoanza kunyesha mwanzoni mwa Januari mkoani Dodoma, hali imekuwa mbaya zaidi baada ya kipande kingine kuharibika upya.

Dk Kigwangalla hatarini CCM


Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla akichangia jambo bungeni siku za hivi karibuni mjini Dodoma. Picha na Maktaba
Dar es Salaam. Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla yuko hatarini kuvuliwa uanachama wa chama hicho, hatua ambayo endapo itachukuliwa itasababisha apoteze nafasi yake ya ubunge.
Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tayari umemjadili Dk Kigwangalla katika vikao vyake vya Kamati za Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa, kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa mbunge huyo.

Dk Slaa: Uswahiba wa JK, Kawambwa unaua elimu


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa 
Mbeya na Arusha. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema, uswahiba wa Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa cha elimu nchini.

SAIKOLOJIA&UTAFITI: Tatizo la wanaume dhaifu linavyohatarisha ndoa

Ni vigumu kufahamu haya, lakini ndio ukweli kuwa kuna kasi ya kuongezeka kwa wanaume dhaifu nchini na ulimwengu kwa ujumla.
Kulingana na taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), tatizo hili la wanaume dhaifu linaongezeka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuendekeza ulevi, matumizi ya tumbaku/sigara, kutokula kwa kuzingatia mchanganyiko wa vyakula (ulaji usiofaa) na watu kutopenda mazoezi.
Hapa nchini hakuna utafiti thabiti uliofanywa lakini nafikiri tutakubaliana kuwa tatizo hili lipo tena ni kubwa, kwani kinyume na hilo kusingekuwa na watu wengi wanaojitangaza kwamba wanatibu. Marekani  wamefanya utafiti, Shirika liitwalo National Ambulatory Medical Care Survey (NAMCS) ambalo linasifika kwa kufanya tafiti mbalimbali za masuala ya afya, linasema kwamba ukionana na Wamarekani 1,000 ujue kwamba 22 ni wanaume dhaifu.

Thursday, 23 January 2014

Mbunge Afariki Dunia


Mke wa Rais Mama Salima Kikwete akiagana na ndugu wa aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Marehemu Said Bwanamdogo wakati alipokwenda kuwafariji nyumbani kwa marehemu, Mbezi Makondeko, Dar es Salaam jana. Picha na Salim 
Dar es Salaam. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepata pigo lingine kwa kuondokewa na Mbunge wa Chalinze (CCM), Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mchungaji jela miaka minne kwa kuuza watu nje

Moshi. Mchungaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean Bamana amehukumiwa kwenda jela miaka minne baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh10 milioni kwa kosa la kujihusisha na biashara ya kusafirisha binadamu.
Akisoma hukumu hiyo mjini Moshi juzi, Hakimu Mkazi Mkoa Kilimanjaro, Sophia Masati alisema iwapo mchungaji huyo atashindwa kulipa faini hiyo atamlazimika kwenda jela miaka minne.
Mchungaji huyo alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuwatorosha wanafunzi wawili wa familia moja hadi Dar es Salaam, ili baadaye awasafirishe hadi nchi za Zambia, DRC na Afrika Kusini.

Wanafunzi watano wafariki dunia Mtwara

Mtwara. Wanafunzi watano wa Sekondari ya Mustapha Sabodo, Kijiji cha Msijute, Wilaya ya Mtwara Vijijini, wamekufa baada ya kugongwa na gari wakikimbia mchakamchaka eneo la shule.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen alisema ajali hiyo ilitokea Jumatatu asubuhi maeneo ya shule hiyo Barabara ya Mtwara-Lindi. Zelothe alisema gari hilo aina ya Mercedes Benz lilikuwa likitoka Mtwara kwenda Lindi.
Alisema waliofariki ni wanafunzi watano na 26 walijeruhiwa, walitibiwa Hospitali ya Rufani Mtwara na kuruhusiwa.

Mafuriko yaikumba Dumila, Kilosa, mamia waathirika na daraja kuvunjika


Wananchi wa Dumila mkoani Morogoro wakitumia uzoefu wao wa kuogelea kujinusuru na mafuriko yaliyotokea jana na kuhatarisha maisha ya watu wengi ikiwa ni pamoja na kuharibu madaraja. Picha na Lilian Lucas 

Morogoro. Mafuriko makubwa yametokea katika Kata ya Dumila, Kilosa mkoani Morogoro na kusababisha mamia ya watu kupoteza makazi huku daraja la Mto Mkundi linaloziunganisha Wilaya za Kilosa na Mvomero likivunjika.

Mwinjilisti adaiwa kumuua mkewe

Bagamoyo. Mwinjilisti wa Kanisa la Anglikana Kijiji cha Gama, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, anadaiwa kumuua mkewe kwa wivu wa mapenzi, kwa kumpiga na panga kichwani kisha kumfukia chini ya magogo aliyoandaa kwenye tanuri la mkaa porini.
Mwinjilisti huyo ambaye ni mkazi wa kijiji hicho, licha ya kazi ya kueneza Injili pia ni mkulima na anajishughulisha na shughuli za kuchoma mkaa porini.

Monday, 20 January 2014

Ndoa ya Obama, Michelle shakani


Obama akiwa na mke wake katika pozi mbalimbali 
Marekani. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya ndani vya Ikulu ya Marekani, wenza hao wamekuwa katika migogoro na Obama alilazimika kusherehekea sherehe za mwaka mpya mjini Hawaii akiwa na binti zake wawili, Sasha na Malia bila kuwepo Michelle.

Serikali yawabeba waliofeli kidato cha pili


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa. Picha na Maktaba 
Dar es Salaam. Wakati Watanzania wakisubiri matokeo ya kidato cha pili mwaka 2013, imebaini kuwa Serikali imetoa agizo kwamba wanafunzi wote waliofeli mtihani huo kuendelea na masomo ya kidato cha tatu, huku wakisoma mafunzo ya kurudia mtihani wa kidato cha pili.

Manchester yanyolewa 3-0 na Chelsea


Ni mara ya kwanza kwa Eto'o kufunga mabao matatu katika mechi moja ya ligi kuu ya Premier

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa matumaini ya mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Premier, Manchester United ya kulihifadhi kombe hilo msimu huu yametumbukia nyongo, baada ya klabu yake kuishinda United kwa magoli matatu kwa moja.

Mapigano zaidi yatokea CAR


Wafanyakazi wa shirika la Msalaba mwekundu wakiwasaidia waliojeruhiwa C.A.R

Kumekuwa na machafuko zaidi katika Jamhuri ya Afrika ya kati, siku moja kabla ya baraza la mpito kumchagua rais mpya wa nchi hiyo.

Iran kuhudhuria mkutano wa Syria-UN


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Iran

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-moon ameikaribisha Iran katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa amani kuhusu Syria utakaofanyika wiki hii, hatua iliyousababisha upinzani mkuu kutishia kuususia mkutano huo.