Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu
Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

Sunday, 26 January 2014

Mwaka 2014 uwe wa waandishi kujirekebisha



Mwaka huu wa 2014, uwe ni mwaka wa kujirekebisha katika uandishi kwani yako matukio mengi ya kihistoria yatakayotokea.
Matukio haya ni maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao, kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya, utayarishaji wa Rasimu ya Katiba ya Tanganyika, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mambo kama hayo.

Msekwa, Kisumo wakoleza moto


 Pius Msekwa>PICHA MAKTABA 
Dar es Salaam. Wakati mjadala wa uteuzi wa mawaziri ukiendelea kupamba moto nchini, makada wakongwe wa CCM, Pius Msekwa na Peter Kisumo wamesema Rais Jakaya Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteua na habanwi na chama, wala mtu yeyote.

Saturday, 25 January 2014

Operesheni ya ujangili yaundiwa mahakama sasa


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema mchakato wa kuwapata wajumbe wa Tume ya Kimahakama ya Kuchunguza Madhara ya Operesheni Tokomeza Ujangili umeshaanza na majina hayo yatawekwa wazi hivi karibuni.

Mvua yaharibu miundombinu reli


Nyumba ikiwa imeharibiawa na mvua iliyoambatana na upepo mkali mkoani Dodona. Mpigapicha wetu 
Dar es Salaam. Wakati timu ya wahandisi ikiendelea kufanya tathimni na marekebisho ya awali ya kipande cha reli reli kilichoharibika eneo la Godegode kutokana na mvua kubwa zilizoanza kunyesha mwanzoni mwa Januari mkoani Dodoma, hali imekuwa mbaya zaidi baada ya kipande kingine kuharibika upya.

Dk Kigwangalla hatarini CCM


Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla akichangia jambo bungeni siku za hivi karibuni mjini Dodoma. Picha na Maktaba
Dar es Salaam. Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla yuko hatarini kuvuliwa uanachama wa chama hicho, hatua ambayo endapo itachukuliwa itasababisha apoteze nafasi yake ya ubunge.
Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tayari umemjadili Dk Kigwangalla katika vikao vyake vya Kamati za Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa, kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa mbunge huyo.