Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, 30 December 2013

Daktari bingwa wa upasuaji aliyepooza viungo



Watu wengi hususani katika jamii za Kiafrika wamekuwa na mtazamo kuwa mtu mwenye ulemavu hawezi kufanya kitu chochote, ambacho kinaweza kuwa na manufaa katika jamii.
Hali hii inachangia kwa kiasi kikubwa walemavu wengi kuishi katika umaskini, huku hata baadhi yao wakiamini kuwa hakuna mchango wowote wanaoweza kuutoa katika jamii, matokeo yake ni kuishia kuombaomba barabarani.
Hata hivyo kwa wenzetu wa mataifa yaliyoendelea ulemavu siyo sababu ya kumfanya mtu ashindwe kufanya shughuli za kijamii au kutoa huduma pale inapohitajika, tena kwa usahihi zaidi wakati mwingine kuliko hata mtu asiyekuwa na ulemavu.
Hilo limedhihirishwa na Ted Rummel raia wa Uingereza ambaye licha ya kupooza mwili wake mpaka kufikia hatua ya kutembelea baiskeli ya wagonjwa, lakini bado ni daktari tegemezi kwenye  idara ya upasuaji  katika hospitali za Progress West na Barnes Jewish St Peters nchini humo.
Daktari huyo ambaye amepooza kuanzia kiunoni mpaka miguuni, ameonyesha kuwa taaluma yake haiwezi kupotea kwa sababu ya ulemavu, alioupata ukubwani hivyo kuamua kuendelea na kazi hiyo katika mazingira magumu.
Licha ya kuishi katika hali ya kupooza kwa muda wa miaka mitatu sasa, Rummel anamudu kuhudumia wagonjwa na kuwafanyia upasuaji ilhali akiwa kwenye kigari maalumu.
Hali ya kupooza mwili haijapunguza ufanisi wa kazi ya Rummel, kwani licha ya kukumbana na changamoto ya kushindwa kusogeza miguu bado ana uwezo mkubwa katika kufanya upasuaji.
Hali hiyo ilivyoanza
Tofauti na watu wengi Rummel alizaliwa mzima kabisa lakini mwaka 2009 akaanza kupatwa na maumivu katika nyonga zake, ingawa hakufikiria kuwa hali hiyo ingeendelea kumsumbua kwa muda mrefu.
Katika mahojiano yake na gazeti la Daily Mail la Uingereza, Rummel anaeleza kuwa aliendelea kuishi na maumivu hayo mpaka Septemba 2010, ambapo ndipo hali ya kupooza ilipoanza rasmi na kujikuta mwili wake ukikosa mawasiliano. Ikamlazimu kuachana na kazi hiyo kwa muda ili apate matibabu na mapumziko ambayo yalichukua kipindi cha miaka miwili, licha ya kutibiwa viungo.
Muda wote aliokuwa katika matibabu Rummel alikuwa karibu sana na familia yake, pamoja na wafanyakazi wengine hali iliyompa faraja na kujikuta akitamani apone haraka ili aweze kurejea kwenye kazi yake.
“Wakati matatizo haya yananikuta nilikuwa tayari nina taaluma na elimu ya kutosha lakini najua wapo wengine ambao yanawakuta wakiwa katika hali mbaya zaidi, ndiyo maana nataka kutumia nguvu na taaluma yangu kuwasaidia,” anasema Rummel na kuongeza;
SOURCE :  gazeti-mwananchi

No comments:

Post a Comment