.jpg)
Mahitajio
|
Utayarishaji
|
Kipimo
|
Kuku bila ya mfupa (kidari)
|
katakata osha
|
1 kilo
|
Kitunguu maji
|
katakata (chop)
|
2
|
Tungule/nyanya
|
“
|
2
|
pilipili mbichi/shamba kijani
|
Saga
|
3
|
Kitunguu thomu/saumu
|
katakata (chop)
|
7-10 chembe
|
Tangawizi mbichi
|
saga
|
1 kipande
|
chumvi
|
kiasi
| |
Pilipili nyekundu ya unga
|
1 kijiko cha chai
| |
Malai (cream)
|
tumia ya tayari
|
1 gilasi
|
Bizari pilau/ jiyrah/cummin
|
1 kijiko cha chai
| |
Gilgilani/Dania/corriander
|
1 kijiko cha chai
| |
Mafuta
|
1/3 kikombe
|
Namna Ya Kupika:
- Weka mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu maji hadi vilainike- Usiache mpaka vikageuka rangi sana.
- Tia kitunguu thomu/saumu na tangawizi mbichi endelea kukaanga.
- Tia vipande vya kuku, endelea kukaanga kidogo
- Tia nyanya, bizari zote, chumvi, pilipili mbichi endelea kukaanga
- Mwishowe tia malai , changanya vizuri, acha ichemke kidogo kuku aive.
- Ongezea malai mwishoni baada ya kuzima moto, changanya vizuri, epua.
No comments:
Post a Comment