Kuku Wa Karai (Pakistani)
.jpg)
Vipimo
Kuku aliyekatwa vipande vipande 5 LB
Mafuta 1 Kikombe cha chai
Nyanya zilizokatwa ndogo ndogo 5 kubwa
Nyanya ya kopo 2 kiijiko vya supu
Thomu na Tangawizi 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi (zipasue katikati) 3 au 5
Bizari ya pilau ya unga (Jeera) 2 vijiko vya chai
Gilgilani ya unga (Dania) 1 kijiko cha chai
Paprika 1 Kijiko cha supu
Bizari ya manjano ya unga 2 vijiko vya chai
Chumvi kiasi
Kotmiri iliyokatwa ndogondogo 1 kikombe kimoja
Pilipili mboga (kijani) 1
Ndimu
2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Tia mafuta katika karai yashike moto vizuri.
2. Tia Thomu na tangawizi kaanga kidogo tu.
3. Tia nyanya, pilipili mbichi, nyanya ya kopo na bizari zote.
4. Mtie kuku na mkaange katika masala hayo.
5. Funika karai na wacha moto wa kiasi, kuku atoe maji yake na apikike.
6. Karibu na kuwiva kuku tia pilipili mboga iliyokatwa vipande vipande, kotmiri na ndimu.
7. Funua karai na endelea kukaanga mpaka awe anakaribia kukauka, muepue na tayari kuliwa.
No comments:
Post a Comment