
Hukumu hiyo ni kama haitekelezeki na pengine mafaili yaliyobeba uamuzi wa mahakama wenye adhabu za vifo, yameendelea kusubiri kusainiwa tangu enzi za uongozi wa awamu ya kwanza wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na hata sasa Rais Jakaya Kikwete.
Watangulizi wengine wa Rais Kikwete ni Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Pili na Mzee Benjamin Mkapa, aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Tatu. Wote wanatajwa kwamba walikuwa wazito kuidhinisha utekelezaji wa hukumu hiyo ya kuondoa uhai wa mtu.
Inaaminika kuwa Serikali za awamu ya kwanza na ya pili zilitekeleza kwa sehemu hukumu hizo, lakini Serikali zilizofuata hazikuwahi kufanya hivyo. Hii inamaanisha kuwa hakuna mtu aliyewahi kunyongwa kwa miaka 18 iliyopita.
Takwimu zilizotolewa na Jeshi la Magereza kwa gazeti hili zinaonyesha kuwa, hadi Oktoba 15, 2013 kulikuwa na watu 364 katika magereza mbalimbali nchini wanaosubiri kunyongwa, baada ya kuhukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Taarifa hiyo iliyosainiwa na Kamishna wa Magezera (CP), Dk Juma Malewa iliweka bayana kuwa hadi wakati huo, wafungwa 86 walikuwa wamekata rufani za kupinga hukumu katika Mahakama ya Rufani Tanzania.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema anasema hawezi kufahamu kwanini Marais wameshindwa kusaini hukumu za vifo kwa muda mrefu, kwani suala hilo lina michakato na mambo mengi ndani yake.
Hata hivyo anaongeza kuwa kutokana na Tanzania kufuata utaratibu wa maadili (moral) katika utawala wake, inaweza kuwa chanzo cha ugumu wa utekelezaji wake.
Hukumu ya Kifo hutolewa chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act. 1985) ambayo inasisitiza kuwa utekelezaji wa hukumu hiyo ni muhukumiwa kunyongwa na siyo vinginevyo.
Kifungu cha 322 cha sheria hiyo kinasema endapo mtu atahukumiwa kwa sheria hiyo, atalazimika kunyongwa mpaka kufa.
Utata wa kusaini
Akifafanua utaratibu wa kufikia hatua ya mwisho katika utekelezaji wa hukumu hiyo, Jaji Werema anasema kabla ya rais kusaini, hukumu hiyo hupitia Mahakama Kuu na ile ya Rufani.
SOURCE : gazeti-mwananchi


hahahaha umetishaaa!!
ReplyDeletebado google tu!
ReplyDeleteHahahahah...google iko njian kk :D
ReplyDeleteHahahahah...google iko njian kk :D
ReplyDelete