Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, 28 December 2013

Wenger atetea matokeo ya vijana wake



Kocha wa Arsenal Arsene Wenger

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger, amesema mpangilio wa mechi ulisababisha
klabu hiyo kucheza mechi nne bila ushindi wowote.

Lakini klabu hiyo ilimaliza ukame huo kwa kushinda mechi ya ya Alhamisi dhidi ya West Ham.
Kocha huyo amesema klabu yake imecheza mechi sita katika kipindi cha siku ishirini na tatu.
''Imekuwa wakati mgumu kwetu, lakini kilichosababisha sisi kutoandikisha matokeo bora ni
wingi wa mechi'' Alisema Wenger.
Arsenal ilianza kampeini yake mwezi huu kwa kuishinda Hull City kwa magoli mawili kwa bila,
 lakini juhudu zao za kujinyakuliwa kombe lao la kwanza kwa zaidi ya miaka tisa, zilianza
kutumbukia nyongo pale ilipozoa alama mbili baada ya kucheza mechi tatu.
Ililazwa 6-3 na Manchester City kabla ya kutoka sare na 
Arsenal pia ililazwa magoli mawili kwa yai na Napoli kwenye mchuano wao wa mwisho wa
 makundi ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya, hata hivyo vijana hao wa Wenger
 walifuzu kwa raundi ya muondoano licha ya matokeo hayo.
Mapema mwezi huu mcheza kiungo wa Arsenal Mikel Arteta alihoji uamuzi wa wasimamizi
wa ligi hiyo wa kuweka mechi yao na Manchester City kuchezwa wakati wa chakula cha
 mchana, akidai kuwa wachezaji walikuwa na muda mfupi sana kujitayarisha baada ya
mechi yao na Napoli siku mbili zilizotangulia.

No comments:

Post a Comment