Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 1 January 2014

Bunge la Uganda lapitisha mswada wa adhabu kwa mashoga

Washiriki katika maadhimisho ya siku ya wapenzi wa jinsia moja Entebbe, Uganda mapema mwaka huu.
Washiriki katika maadhimisho ya siku ya wapenzi wa jinsia moja Entebbe, Uganda mapema mwaka huu. Bunge la Uganda Ijumaa lilipitisha mswada ambao utafanya baadhi ya vitendo vya ngono kati ya watu wa jinsia moja kupewa adhabu ya kifungo cha maisha jela.


Mahojiano ya Halima Athumani na Mkamiti Kibayasi




Mswada huo awali ulishtumiwa na  makundi ya kutetea haki pamoja na serikali za Magharibi ikiwemo Marekani kwa sababu ulijumuisha adhabu ya kifo.

Mswada uliopitishwa Ijumaa unatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa yeyote atakayehukumiwa kwa kile ilichosema ni "vitendo vilivyopita mipaka"vya ngono kati ya watu wa jinsia moja.

Waziri Mkuu Amama Mbabazi alikaririwa akisema kuwa serikali ya Uganda itafanya mashauriano zaidi kuhusu mswada huo ambao unahitaji kutiwa saini na Rais Yoweri Museveni kabla ya kuwa sheria kamili nchini humo.


SOURCE : VOA

1 comment: