
Vipimo
Unga 2 vikombe vya chai
Hamira 1 ½ Kijiko cha chai
Samli 1 Kijiko cha Supu
Maji 1 ½ kikombe cha chai (kiasi)
Mafuta ya kukaangia kiasi
Shira 1 kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya unga Hamira, Samli, maji, kisha vuruga kulainisha unga hadi uwe hauna madonge na mwepesi kiasi.
- Funika unga uumuke. Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto.
- Ziepue na zichuje mafuta.
- Weka kaimati katika bakuli au sahani kisha mwagia Shira zikiwa tayari.
Shira:
Sukari 2 vikombe
Maji 1 kikombe
Zaafarani 1 kijiko cha chai
Hiliki ¼ kijiko cha chai
Arki (rose flavour) 3-4 matone
Namna Ya Kutayarisha Shira
- Roweka zaafarani katika kibakuli kwa maji ya moto kiasi ya vijiko 3 vya supu.
- Tia sukari na maji katika kisufuria kidogo, acha kwenye moto ichemke pole pole hadi iwe nzito kidogo.
- Tia zaafarani, hiliki na arki ikiwa tayari kumwagiwa juu ya kaimati.
No comments:
Post a Comment