Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana alitinga
mahakama kuu kupinga kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao
ambacho kilikuwa kikutane leo.Hii ni kauli yake baada ya mahakama kumpa ushindi;
"Jana tulikwenda mahakamani kwa ajili ya jambo moja tu kutaka haki itendeke kwa sababu mahakaama ndiyo chombo cha juu kabisa kwenye nchi yetu cha kuweza kutenda haki mara baada ya kamati kuu ya chama changu kufanya maamuzi ya kunivua nafasi zangu ambayo niliandikiwa makosa 11
"Nilikata rufaa kwenye baraza kuu la chama ili baraza
kuu liweze kuona kama kamati kuu ilifuata taratibu za chama kufikia maamuzi yale
japo mimi
naamini haijafuata taratibu za chama lakini kwa bahati mbaya viongozi wangu wa chama changu wameamua kuendelea na kikao cha kamati kuu.
naamini haijafuata taratibu za chama lakini kwa bahati mbaya viongozi wangu wa chama changu wameamua kuendelea na kikao cha kamati kuu.
"Hawajajibu barua yangu ya nia ya kukata rufaa na
kuweza kupatiwa taarifa na mwenendo wa kikao ili niweze kukata rufaa kwa mujibu
wa chama. Kwa hiyo nimekwenda mahakani ili mahakama iweze kutoa maamuzi ya mimi
kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa na kujadiliwa.
"Nashukuru Jaji John Utamwa ametoa amri ya muda ya
kuzuia kamati kuu ya chama kunijadili mpaka hapo Chadema watakapoweza kujibu
hoja zilizotolewa na mwanasheria wangu Albert Msando.
"Leo tunarudi mahakamani kwa ajili ya kuendelea na
kuweza kupokea majibu kutoka Chadema lakini kikao cha leo kamati kuu imezuiliwa
na mahakama kujadili hoja yoyote inayonihusu,lakini pia mapingamizi yote
mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu aliyokua ameyaweka dhidi ya mwanasheria wangu
Jaji ameyatupilia mbali kwa hiyo kesi inaendelea.
"Muhimu katika hili ni haki na mimi kama mtu ambaye
siku zote natetea haki sasa ni fursa yangu kutetea haki yangu mwenyewe ya kuweza
kusikilizwa ya kutumia taratibu zote za chama katika hali ya kawaida baraza kuu
la chama liitwe kwanza lijadili jambo hili kabla ya kikao cha kamati kuu
kuitwa".
SOURCE : Mpekuzi






No comments:
Post a Comment