Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na mashine ya kutolea risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa
amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanyabiashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.Nukuu ya taarifa kutoka PamojaPure blog —
Haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa majambazi hao walikuwa watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG.
Baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba
Mmoja wa mashuhuda alisema, “Niliona watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia mlio wa risasi na kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa kasi kutokea upande wa mtaa wa Gerezani na kisha mlio wa pili wa risasi ulikika tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule "Muhindi" na baada ya hapo kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana lile begi na kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza kufunga maduka yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisi.”
SOURCE : wavuti





No comments:
Post a Comment