
Wananchi wakiangali mojawapo ya nyumba zaidi ya 20 zilizokuwa katika kijiji cha Kikundi Kata ya Kiroka, ambazo zinazodaiwa kubomolewa kwa amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya Morogoro Vijijini mkoani Morogoro.Picha na Juma Mtanda
Meatu. Kaya 83 zimeezuliwa kutokana na mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali, huku takriban ekari 15 za mazao mbalimbali zikiharibiwa.
Tukio hilo lilitokea Januari 8 saa 1:00 jioni kijiji na Kata ya Mwandoya, wilayani Meatu, hali iliyosababisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti kutembelea waathirika.
Akisoma taarifa ya awali iliyoandaliwa na Kitengo cha Maafa cha Wilaya, Naibu Katibu Tawala Wilaya ya Meatu, Mossa Lutani alisema baada ya kupata taarifa ya maafa hayo timu ya wataalamu ilitumwa kufanya tathmini. Lutani alisema timu hiyo ilishirikiana na uongozi wa kata, vijiji na viongoji vyote vilivyokumbwa na maafa kuzungukia maeneo yaliyoathiriwa kubaini jinsi waathirika wanavyoweza kusaidiwa.
Alisema vitongoji vya kijiji vilivyokumbwa na maafa ni sita, kati ya vinane navyo ni Madukani, Mabondeni, Itugutu, Manasubi, Kanisani na Kisimani na kwamba, waathirika wakubwa ni kaya tano ambazo nyumba zimebomolewa na kuezuliwa paa kabisa.
Lutani alisema Tabu Mazingo ameripotiwa kufa maji akijaribu kuvuka mto kutoka Kijiji cha Mwandoya kwenda Mwandaya, huku wengine watatu wakijeruhi wa kwa kuangukiwa na kuta.
Akizungumza na waathirika, Mabiti alisema Serikali inafanya jitihada kuhakikisha huduma zote za jamii kama miundombinu ya barabara zinatengenezwa na visima vilivyoharibiwa kusafishwa vizuri ili kupata maji salama.
Pia, Mabiti aliwataka wananchi kupanda miti ya kutosha, kwani Meatu haina miti ya kutosha.
SOURCE : Gazeti-Mwananchi
No comments:
Post a Comment