Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, 20 January 2014

Rais wa Ukraine kuanzisha mazungumzo ya amani

Maandamano nchini Ukraine
Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych, amesema kuwa ataunda tume maalum ya kushirikisha pande zote zinazozozana nchini humo kusuluhisha ghasia za kisiasa ambazo zimeendelea kwa majuma kadhaa.

Tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya mapambano makali katika mji mkuu wa Kiev, ambako magari yaliteketezwa na grunedi za kuwashtua waandamanaji kutumiwa wakati polisi wa kupambana na ghasia wakikabiliana na wapinzani wa Serikali.
Makumi ya watu wamejeruhiwa katika makabiliano hayo.
Kiongozi wa Upinzani, Vitali Klitschko, alisema kuwa amemwomba Rais ajiuzulu na kuitisha Uchaguzi Mkuu.
Marekani imetoa wito kusitishwa kwa mapigano mara moja. Mapigano yalianza nchini humo miezi miwili iliyopita, baada ya Rais wa Taifa hilo kupuuza mkataba wa biashara na Jumuiya ya Ulaya na badala yake kuimarisha uhusiano na Urusi.

Source: BBC swahili

No comments:

Post a Comment