Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 1 January 2014

Saladi Ya Viazi (Aina 1)

 
Vipimo




Viazi (mbatata)                                          ¼ kilo (kiasi viazi 5)   au vitano

Limau au ndimu au siki                                  ½ kikombe

Vitunguu nyasi   (spring onions)                    4-5 miche                        

Mafuta ya zaituni (oliven oil)                          ½ kikombe  

Chumvi                                                          Kijiko cha chai kimoja na nusu




Namna Ya Kutayarisha Na Kupika


  1. Chemsha viazi na  maganda yake hadi viive bila ya kuvurujika

  1. Viache vipowe kisha chambua viazi ukatekate slesi au vidogodogo, mimina ndani ya bakuli kubwa.


  1. Katakata vitunguu tia kwenye viazi, tia chumvi na mafuta ya zaituni, limau  kisha vichanganye  uzuri.

  1.  Onja chumvi na limau ukiona yametokeza ladha basi saladi tayari kwa kuliwa. 


Kidokezo;

  1. Hii ni saladi huliwa sana wakati wa majira ya joto  (summer). Waweza kula saladi hii kwa nyama ya kuchoma au samaki.

  1. Unaweza kuhifadhi kwenye friji  kwa matumizi ya siku ya pili.

No comments:

Post a Comment