
Vipimo
Peya 2
Maziwa 4 gilasi
Maji 1 gilasi
Sukari kiasi
Lozi 1/4 kikombe
Namna ya Kutayarisha:
1. Menya peya, toa kokwa.
2. Roweka Lozi kisha umenye maganda na ukate kate ndogo ndogo au tumia za tayari.
3. Tia peya, maziwa na sukari katika mashine ya kusagia (blender) na vipande vya barafu kidogo usage.
4. Ikiwa nzito bado ongeza maji
5. Mimina katika gilasi, pambia lozi.
No comments:
Post a Comment