
VIPIMO
Spaghetti 500 gramu (gms)
Chumvi Kiasi
Mafuta ya kukaangia 1/4 kikombe
Kitungu kilichokatwa 1 kiasi
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Sosi ya pilipili (HP sauce) 1 kijiko cha chai
Siki 3 Vijiko vya supu
Sosi ya soy 3 vijiko vya supu
Pilipili mboga kijani na nyekundu 1 kila moja (iliyokatwa)
Mchanganyiko wa mboga za barafu 1 magi
Kuku au nyama isio na mifupa iliyokwishapikwa kiasi upendavyo
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Chemsha spaghetti kwa chumvi na mafuta kidogo kwa kufuata maagizo yake katika karatasi.
2. Yakishawiva mwaga maji kwa kuchuja na uweke kando.
3. Katika sufuria kubwa , tia mafuta na kaanga vitungu , mchanganyiko wa mboga , chumvi na pilipili hadi mboga iive kidogo na sio kuvurujika.
4. Tia na ukaange vilivyobaki isipokuwa spaghetti na kuku unaziwacha mwisho.
5. Iwache dakika 2 hivi kwenye moto mdogo na itakuwa tayari kuliwa.
No comments:
Post a Comment