
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe.
Dar es Salaam. Hatima ya maombi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, itajulikana leo wakati Mahakama Kuu ya Tanzania, katika Kanda ya Dar e s Salaam itakapotoa uamuzi kuhusu maombi hayo.
Uamuzi huo unatarajiwa kutoelewa saa 4:00 asubuhi na Jaji John Utamwa, anayesikiliza shauri hilo.
Katika maombi hayo namba 1 ya mwaka huu, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, anaiomba mahakama iizuie Kamati Kuu ya Chadema, kumjadili au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake.
Zitto kupitia kwa wakili wake, Albert Msando, ameiomba mahakama itoe zuio hilo la muda hadi kesi yake ya msingi namba 1 ya mwaka 2014 aliyoifungua mahakamani itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Hata hivyo, Chadema kupitia kwa mawakili wake, Tundu Lissu na Peter Kibatala, walipinga maombi hayo wakidai kuwa hayajakidhi vigezo vya kupewa zuio la muda wanaloliomba.
Ikiwa Mahakama Kuu katika uamuzi wake leo itakubaliana na hoja za maombi ya Zitto na kutoa zuio la muda, Chadema haitaweza kumchukulia hatua zozote wala kujadili kuhusu uanachama wake, hadi kesi yake ya msingi itakapomaliza.
Katika kesi ya msingi, Zitto anaiomba mahakama ikizuie chama hicho kumchukulia hatua
SOURCE : Gazeti-Mwananchi
No comments:
Post a Comment