Imesimuliwa na sahaba Abu Said al khudry radhi za Allah ziwe juu yake kwamba amesema Mtume wa Allah rehma na Amani ziwe juu yake "Atakaesoma suratul Kahfi siku ya Ijumaa, Allah atamuangazia nuru baina ya ijumaa mbili". Imepokelewa na Imam Nasai na Bayhaqy.
Katika sunna za siku ya ijumaa, sunna ambayo imetiliwa mkazo ni kusoma suratul kahfi kwani atakaesoma Allah humuangazia nuru kwa wiki nzima. Na ni nani asietaka kumurikwa na nuru ya Allah isiyozimika? Mambo yake yakawa mepesi? Kwa masikitiko umma uko mbioni kutafuta dunia na kusahau akhera. Watu tukashindwa kuweka robo saa au nusu saa kwa ajili ya kusoma suratul kahfi. Tumekua wagumu hadi tunampangia Allah muda wa kumuabudu, muda ambao yeye ndo katutunukia, subhanallah vipi akiuzuia muda wake nani wakumlaumu zaidi ya nafsi zetu, na kuzuia kwake muda ni pale malakul-maut atakapofika kuchukua amana, na tumpe Mola wetu muda wetu wala tusimpangie robo saa au nusu saa. Allah atuwafikishe.
ALLAH TUJAALIE WALE WENYE KUAMBIWA MAZURI NA KUYAFANYIA KAZI NA KUKATAZWA MABAYA NA KUYAWACHA"Aaamin.
“NA KUMBUSHA, KWANI UKUMBUSHO HUWAFAA WAUMINI”(51:55).
No comments:
Post a Comment