Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, 27 December 2013

KISA CHA MTUME MUHAMMAD(SWALLA ALLAHU ALAYHI WASALLAM)NA BIBI KIZEE

Siku moja Mtume Muhammad(swalla Allahu alayhi wasallam)alitoka nje ya mji kwa ajili ya shughuli zake. Wakati yupo huko njiani akakutana na bibi mmoja mtu mzima akiwa amebeba mzigo mzito kabisa.Mtume(swalla Allahu alayhi wasallam) akamuendea yule bibi na kumsaidia mzigo wake.Wakati wanaelekea nyumbani kwa yule bibi, yule bibiakamwambia Mtume kijana inaonekana ni mtu mzuri na mwenye tabia njema.Nakunasihi sana ujiepushe na mtu mmoja ambae ameingia katika mji wetu.Huyu mtu mshirikina,mwendawazimu,mfitinishaji almuhimu majina yote mabaya ya kumtukana Mtume aliyamaliza.Ila Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) hakunyanyua mdomo wake kumjibu vibaya yule bibi au kuuweka chini mzigo alokuwa
akimsaidia.Walikwenda mpaka wakafika kwake yule bibi.Yule bibi akamwambia Mtume(swalla Allahu alayhi wasallam) je unaitwa nani ewe kijana?Mtume akamwambia naitwa Muhammad.Bibi uso wake ukatahayari,hajui wapi auweke uso wake maana alimaliza matusi yote kumtukana mtu ambae alikuwa akimsaidia.Kwani jina la Mtume alilikuwa akilisikia bila ya kumjua.Kwa kitendo hicho cha Mtume yule bibi akatoa shahada na kumkubali kuwa Mtume (swalla Allahalayhi wasallam)alikuwa ni Mtume wa kweli.Hakuna kilichomfanya aukubali uislamu isipokuwa ni kuona tabia njema za Mtume Muhammad (swallah Allahu alayhi wasallam).
Ndugu zangu wakiislamu tujipambeni na tabia nzuri na kioo chetu kiwe ni Mtume Muhammad(swalla Allahu alayhi wasallam) Allah anatuambia ndani ya Quraan “Kwa yakini umekuwa mfano mzuri kwenu katika mwendo wao, kwa anaye mtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho..”(60:6).Tabia zake tu ziliwafanya wengi wasilimu.Huyo ndie kipenzi cha Umma (swalla Allahu alayhi wasallam).Na sisi tuige mfano matendo yake kwa hakika kufanya hivyo ni sababu ya kupata ridhaa za Allah.Na tusiige sifa mbaya za waimbaji,waigizaji na wengineo ambao hutupelekea kuingia pabaya.Allah atunusuru na ajaalie tabia zetu ziwe njema.Aaamin.
ALLAH TUJAALIE WALE WENYE KUAMBIWA MAZURI NA KUYAFANYIA KAZI NA KUKATAZWA MABAYA NA KUYAWACHA"Aaamin.
“NA KUMBUSHA, KWANI UKUMBUSHO HUWAFAA WAUMINI”(51:55).

No comments:

Post a Comment