Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, 27 December 2013

KILIO CHA OMAR IBN ABDUL AZIZ

Siku moja Omar Ibn Abdul Aziz alisikilikana analia kwa sauti na kushindwa kujizuia.Jirani yake akaenda kumuuliza “Je ni kipi kimekusibu hadi unalia?”Omar Ibn Abdul Aziz akamwambia ”Hakuna kilichoniliza isipokuwa aya hii ndani ya Quraan,Allah(subhanahu wataala)anasema “…Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi, na kundi jengine Motoni”(42:7).Najiuliza ndani ya nafsi yangu je nitakuwa katika kundi lipi kati ya haya mawili?
Ndugu zangu wa kiislamu na sisi tukae tupate mazingatio,siku yatakapogaiwa makundi haya mawili je tutakuwepo katika kundi lipi?Hakuna kitakachotusalimisha na kuwemo katika kundi la motoni ila kwa kutenda mema na kuwa wachamungu.
Tunamuomba Allah atujaalie kuwa ni katika kundi la watu wa peponi na atuepushe na adhabu ya moto.Aaamin.
“Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa.”(2:281).

No comments:

Post a Comment