Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 1 January 2014

Chapati Za Maji (Pancakes) Za Blue Berries na Asali

   
Vipimo


Unga                                                            2 vikombe

Baking Powder                                             2 vijiko vya chai

Sukari                                                          ½ kikombe

Yai                                                               1

Maziwa                                                        1 ¼ kikombe

Maziwa ya mvuke (evaporated milk)            ¾ kikombe

Siagi                                                            1 Kijiko cha supu


Mjazo

Blue berries

Asali


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika


  1. Tia unga, baking powder na sukari katika bakuli.
  
  1. Weka yai, maziwa yote na siagi katika bakuli jengine na upige kwa   wiski  (whisk – mwiko wa kupigia mayai) hadi ichanganyike, kisha changanya katika unga na endelea kupiga kwa wiski hadi uchanganyike vizuri na uwe nyororo.
  
  1. Weka motoni kikaango kisichoganda (non-stick frying pan), moto baina ya mdogo na wastani.
  
  1. Chota kwa mwiko kiasi nusu 1/3 kikombe (au takriban ½ kikombe) mimina katika kikaango.
  
  1. Subiri itoe viputo (bubbles) kisha geuza upike upande wa pili. Pande zote ziive kugeuka rangi ya dhahabu.
  
  1. Epua weka kando huku ukimaliza kupika mikate mingine.
  
  1. Panga katika sahani na kila juu ya mkate tia blue berries na asali, panga nyigninezo juu yake hivyo hivyo kiasi utakavyotaka kuhudumia.

Kidokezo:

  1. Unaweza kutumia matunda mengine.

  1. Kipimo Cha kiasi mikate 15

No comments:

Post a Comment