
VIPIMO
Karoti iliyoparuzwa 3 vikombe vya chai
Sukari 2 vikombe vya chai
Maziwa 2 vikombe vya chai
Lozi au korosho 1 kikombe cha chai
zilizokatwa ndogo ndogo
Hiliki ½ kijiko cha chai
Samli 4 vijiko vya chai vidogo
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Kaanga lozi kwa ile samli kidogo ziweke pembeni.
- Tia maziwa, hiliki na sukari kwenye sufuria chemsha ikisha chemka mimina Karoti.
- Chemsha mpaka ikauke maziwa tia lozi.
- Mimina kwenya trei.
- Ikisha kupoa kata vipande. Tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment