Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 1 January 2014

Chapati Za Maji (Pancakes) Za Stroberi Na Chokoleti

  
Vipimo


Unga                                                            2 vikombe

Baking Powder                                             2 vijiko vya chai

Sukari                                                          ½ kikombe

Yai                                                               1

Maziwa                                                        1 ¼ kikombe

Maziwa ya mvuke (evaporated milk)            ¾ kikombe

Siagi                                                            1 Kijiko cha supu


Mjazo

Jamu ya Stroberi                                         1 kijiko cha chai

*Chokoleti                                                   kiasi

Sukari ya unga                                             1 kijiko cha chai


Yayusha baadhi ya chokoleti na kipande kimoja acha kando



Namna Ya Kutayarisha Na Kupika


  1. Tia unga, baking powder na sukari katika bakuli.
  
  1. Weka yai, maziwa yote na siagi katika bakuli jengine na upige kwa   wiski  (whisk – mwiko wa kupigia mayai) hadi ichanganyike, kisha changanya katika unga na endelea kupiga kwa wiski hadi uchanganyike vizuri na uwe nyororo.
  
  1. Weka motoni kikaango kisichoganda (non-stick frying pan), moto baina ya mdogo na wastani.
  
  1. Chota kwa mwiko kiasi nusu 1/3 kikombe (au takriban ½ kikombe) mimina katika kikaango.
  
  1. Subiri itoe viputo (bubbles) kisha geuza upike upande wa pili. Pande zote ziive kugeuka rangi ya dhahabu.
  
  1. Epua weka kando huku ukimaliza kupika mikate mingine.
  
  1. Panga katika sahani na fanya sandwich kwa kutia jamu ya stroberi.
  
  1. Nyunyizia chokoleti juu yake na weka kipande kimoja cha  chokoleti juu yake.

  1. Nyunyizia sukari ya unga ikiwa tayari


Kidokezo:


Kipimo Cha kiasi mikate 15

No comments:

Post a Comment