
Vipimo
Unga 2 vikombe
Baking Powder 2 vijiko vya chai
Sukari ½ kikombe
Yai 1
Maziwa 1 ¼ kikombe
Maziwa ya mvuke (evaporated milk) ¾ kikombe
Siagi 1 Kijiko cha supu
Mjazo
Sosi ya stroberi (strawberry filling)
Lozi
Aisikirimu (icecream) ya stroberry
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia unga, baking powder na sukari katika bakuli.
- Weka yai, maziwa yote na siagi katika bakuli jengine na upige kwa wiski (whisk – mwiko wa kupigia mayai) hadi ichanganyike, kisha changanya katika unga na endelea kupiga kwa wiski hadi uchanganyike vizuri na uwe nyororo.
- Weka motoni kikaango kisichoganda (non-stick frying pan), moto baina ya mdogo na wastani.
- Chota kwa mwiko kiasi nusu 1/3 kikombe (au takriban ½ kikombe) mimina katika kikaango.
- Subiri itoe viputo (bubbles) kisha geuza upike upande wa pili. Pande zote ziive kugeuka rangi ya dhahabu.
- Epua weka kando huku ukimaliza kupika mikate mingine.
- Panga katika sahani na kila juu ya mkate pakaza sosi ya stroberi kisha tandaza lozi kisha weka aisikirumu pembeni ikiwa tayari.
Kidokezo:
- Unaweza kutumia jamu ya stroberi
- Kipimo Cha kiasi mikate 15
- Weka aisikirimu wakati tayari kuliwa isiyayuke pindi ukiweka mapema.


No comments:
Post a Comment