Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 1 January 2014

Halwa - Halua

           
Vipimo

Uwanga (corn flour)
¼ kilo (250g)
Sukari
2 kilo
Samli au mafuta ya kupikia
2 kilo 3lita
Hiliki
2 vijiko vya supu
Kungumanga
1 kijiko
Majani ya chai
10 vijiko au teabags
Arki ya rose
1kijiko
zafarani
½ kijiko cha chai
maji
3 ½ lita au birika mbili za maji moto
Lozi (almond)
½ Kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.     Roweka majani ya chai vikombe 2 vya  maji ya moto upate rangi iliyokoza.
2.     Chuja kwenye sufuria kubwa, mimina maji lita tatu na nusu  au birika ya umeme mawili ya  maji.
3.     Kwenye hayo maji  tia, sukari, iliki, kungumanga,maji ya majani ya chai,zafarani na arki. Wacha mpaka ichemka.
4.     Wakati sufuria ipo jikoni chukua kibakuli utie unga wa conflour changanya na maji ya kawaida vikombe viwili.
5.     Mchanganyiko ukishakuaanza kuchemka mimina ule unga uliouchanganya  na maji, koroga bila kuachia mkono kwa kutumia mwiko mrefu.
6.     Ukiona mchanganyika umeshashikana sawa sawa, mimina samli  vikombe viwili.
7.     Endelea kukoroga bila ya kuachia na mchanganyiko ukiwamzito  tia samli na endelea kukoroga. Muda wote koroga kwa mzunguko wa kuelekea upande mmoja tu kushoto au kulia. ( clockwise au anticlockwise)
8.     Utaendelea kufanya hivyo kwa masaa mawili mpaka mafuta yajitenge mbali na halua. Na yataanza kuruka ruka.
9.     Ili kujua kama halua tayari imeshawiva, ukiwa unakorogo chota kwenye kijiko kidogo uiache ipoe, kama inaonekana ipo ngumu baada ya kupoa , basi itakuwa tayari.la nilaini sana iwache kwenye moto huku unaendelea kukoroga mpaka iwe ngumu kwenye kijiko ikipoa.
10.  Ikiwa tayari tenganisha mafuta yote na  halua.
11.  Baada ya hapo itie kwenye trays au vibakuli ya ufuniko na uipambie kwa kumwagia juu lozi zilizokatwa katwa.

Kidokezo: unaweza kupambia lozi , njugu au ufuta juu. Pia unaweka kwenye mchanganyiko vitu hivyo  pale unakoroga ikiwa ipo jikoni.

No comments:

Post a Comment