
Vipimo
Unga wa ngano 1 Kikombe
Sukari 2 Vijiko vya supu
Baking powder 1 Kijiko cha supu
Chumvi 1/2 Kijiko cha chai
Mayai 2
Maziwa 2 Vikombe
Ngano yakupikika haraka(oats) 1 Kikombe
Siagi (iliyoyayushwa),au mafuta 2 Vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Weka unga, sukari, baking powder na chumvi katika bakuli.
2. Kwenye bakuli jengine, piga mayai kidogo changanya maziwa, ngano na siagi na iache ikae dakika mbili.
3. Kisha changanya pamoja na mchanganyiko wa unga.
4. Weka chuma kisichoganda (non stick) kipate moto.
5. Paka mafuta kidogo kisha tumia kijiko cha kupakulia tia mchanganyiko iwe duara (kama vibibi).
6. Itakapoanza kufanya mapovu juu, geuza upande wa pili hadi iive.
7. Endelea hivyo hivyo mpaka umalize unga wote.
8. Panga kwenye sahani na tayari kuliwa na asali au shira ya sukari pekee au shira ya matunda kama maple syrup.
Kidokezo
Unaweza kutumia chuma kikubwa kufanya viduara 3 au 4 kwa mara moja
No comments:
Post a Comment