Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, 7 January 2014

Hamas yapinga mapendekezo ya John Kerry

Msemaji wa HAMAS, Sami Abu Zuhri










Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kuwa inapinga mapendekezo yaliyotolewa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kwa ajili ya kutatua mzozo kati ya pande mbili za Palestina na Israel.
Moja ya mapendekezo yaliyotolewa na John Kerry ni kuwa, Quds iwe mji mkuu wa pamoja kati ya serikali mbili za Palestina na Israel. Sami Abu Zuhri msemaji wa harakati ya Hamas amesema leo kuwa harakati hiyo kimsingi inapinga suala la kufanya mazungumzo na utawala wa Kizayuni. Abu Zuhri ameongeza kuwa ujumbe wa Hamas kwa John Kerry Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ni huu kwamba, mapatano ya aina yoyote yatakayopatikana katika mazungumzo hayawezi kuwa na umuhimu kwa wananchi wa Palestina ambao kiujumla wanapinga mazungumzo ya mapatano kati yao na utawala wa Kizayuni. Marekani pia imetoa pendekezo kwa viongozi wa Israel kwamba, vifaa vya kisasa kama satalaiti na ndege zisizo na rubani zipelekwe katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la bonde la Jordan badala ya kuwatuma wanajeshi wa Israel katika eneo hilo na pia wanajeshi wa utawala huo wawe katika vivuko vya mpakani kwa miaka kadhaa tu. John Kerry Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni katika duru mpya ya safari yake katika eneo.
SOURCE : Iran Swahili

No comments:

Post a Comment