Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, 7 January 2014

Bashir: Tuko tayari kusaidia mgogoro wa Sudan Kusini

Bashir: Tuko tayari kusaidia mgogoro wa Sudan Kusini

Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan amesema leo kuwa nchi yake iko tayari kuisaidia kwa hali na mali nchi jirani ya Sudan Kusini ili kutatua mgogoro unaoendelea kutokota kwa hivi sasa nchini humo.

Rais al-Bashir amesema hayo kwenye mkutano wake na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini mjini Juba leo Jumatatu. Rais Bashir amesema mgogoro wa Sudan Kusini unaathiri mambo mengi huko Khartoum hususan masuala ya kiuchumi. Rais wa Sudan amesema kwenye mazungumzo hayo kwamba, nchi yake inaunga mkono jitihada zinazofanywa na Jumuiya ya IGAD za kuutafutia ufumbuzi mgogoro ulioko Sudan Kusini.
Huku hayo yakijiri, China imetaka pande zinazohasimiana huko Sudan Kusini kusitisha mapigano mara moja na kutoa fursa kwa mazungumzo ya amani kufanyika. Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amesema mjini Addis Ababa, Ethiopia kuwa lazima kuwe na usitishwaji mapigano ili mazungumzo yafanikiwe. China ni muwekezaji mkubwa katika sekta ya mafuta nchini Sudan Kusini
SOURCE : Iran Swahili

No comments:

Post a Comment