
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena wamezitihumu nchi za Uganda na Rwanda kuwa zilikuwa zikiwaunga mkono waasi wa M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya onyo kutoka kwa umoja huo.
Kwenye ripoti mpya inayotarajiwa kuchapishwa wiki ijayo, wataalamu wa UN wanasema Kampala na Kigali zilikuwa zikitoa misaada ya silaha pamoja na mafunzo ya kijeshi kwa waasi hao nyuma ya pazia lakini kidhahiri zilikuwa zikisema zinapinga uasi DRC. Ripoti hiyo inasema kwamba katika kipindi fulani Rwanda ilitoa msaada wa moja kwa moja wa kijeshi kwa M23. Kuhusiana na suala hilo, ripoti hiyo inafafanua kwamba, mwezi Agosti mwaka uliopita wanajeshi wa Rwanda walivuka mpaka na kuingia upande wa DRC kwa lengo la kuwasaidia waasi wa M23.
Wachambuzi wengi wanaitakidi kuwa, kuchapishwa ripoti hiyo wiki ijayo kutahuisha tena uhasama wa kisiasa kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande mmoja na Rwanda na Uganda kwa upande wa pili.
SOURCE : Iran Swahili
No comments:
Post a Comment