
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imesisitiza kuwa vitisho na mashambulio ya kigaidi hayataifanya iache kuunga mkono serikali ya Rais Bashar la Assad wa Syria.
Katika taarifa yake Hizbullah, imesema kwamba, harakati
hiyo haiwezi kutishwa na shambulizi la bomu la hivi karibuni lililofanywa mjini Beirut na kundi lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida.
Matamshi hayo yametolewa baada ya kundi la kigaidi linaloitwa 'Utawala wa Kiislamu Iraq na Sham (ISIL) kutangaza jana kuwa, ndilo lililotekeleza shambulizi la mlipuko wa bomu la kutegwa garini katika kitongoji cha kusini mwa Beirut ambapo watu wawili waliuawa.
Kundi hilo la kigaidi pia limedai kwamba, limejipenyeza katika mfumo wa usalama wa Hizbullah ili kushambulia ngome za harakati hiyo.
SOURCE : Iran Swahili


No comments:
Post a Comment