
Vipimo
Makoroni 500 gms
Mafuta ya kuchemshia makoroni ¼ kikombe
Nyama ya kusaga ½ kilo
Mafuta ¼ kikombe
Vitunguu vilivyokatwa (chopped) 3
Tomato iliyokatwa ndogo ndogo 1
Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo 1
Thomu 1 kijiko cha supu
Pilipili manga 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Vipimo Vya Bashamela
Unga 5 vijiko vya supu
Siagi 3 vijiko vya supu
Maziwa 5 vikombe
Jibini (Cheese) Ya Malai (Cream) 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Makaroni
1- Chemsha macaroni na mafuta hadi yawive mwaga maji na chuja.
Sosi Ya Nyama
1. Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi.
2. Tia thomu kaanga kidogo.
3. Tia nyama, chumvi na pilipili kaanga hadi nyama iwive.
4. Ukipenda tia kipande cha maggi ukichambue kisha changanya vizuri.
5. Zima moto, tia nyanya na pilipili mboga.
Bashamela
1. Katika sufuria tia siagi weka katika moto.
2. Tia unga na kaanga ugeuke rangi uwe rangi brauni khafifu.
3. Tia maziwa na haraka haraka ukoroge kwa mchapo wa mayai kutoa madonge.
4. Tia cheese. Ikiwa madonge hayakutoka tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage kisha rudisha kidogo katika moto mdogo mdogo na huku unakoroga kwa mchapo wa mayai.
Kutayarisha Kuyapika
1. Tia nusu ya sosi ya nyama chini ya bakuli la kupikia katika oveni.
2. Tia nusu makaroni na mwagia nusu ya bashamela.
3. Tia tena nusu nyingine ya nyama kisha tena makaroni kisha tena bashamela.
4. Pika (bake) katika moto wa 400 Deg kwa muda wa dakika 15-20 hadi bashamela igeuke rangi kidogo.
5. Epua ikiwa tayari kuliwa.
No comments:
Post a Comment