
Vipimo
Makaroni ya aina yoyote 375 gms
Nyama ya kuku iliokatwa vipande 1 Lb
Kitunguu 1
Thomu na tangawizi 1 Kijiko cha supu
Mdalasini ¼ Kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Pilipili manga ya unga ¼ Kijiko cha chai
Ndimu ½
Kidonge cha supu 1 Kidonge
Mboga za barafu 2 Vikombe vya chai
Namna Ya kutayarisha na Kupika
1. Katika sufuria, mtie kuku, chumvi, pilipili manga, thomu na tangawizi, kitunguu, mdalasini na kidonge cha supu.
2. Weka katika moto na mpike hadi awive.
3. Kisha utoe mifupa na uchambue nyama ndogo ndogo weka kando.
4. Chemsha makaroni kwa chumvi na mafuta kidogo kwa kufuata maagizo yake katika pakiti.
5. Karibu na kuiva tia mboga za barafu na ziache dakika moja hivi.
6. Ikishaiva mwaga maji kwa kuchuja na weka katika sufuria.
7. Changanya na kuku uliomtayarisha na kamulia ndimu na itakuwa tayari kwa kuliwa na kechapu ya nyanya (tomato ketchup).
No comments:
Post a Comment