
Vipimo
Makaroni 500 gms
Vipimo Vya Kuku
Kuku 3 LB
Thomu na tangawizi iliyosagwa 2 vijiko vya supu
Tanduri masala 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Mtindi (yoghurt) 2 vijiko vya supu
Jiyrah (cummin powder) 1 kijiko cha chai
Dania (coriander powder) 1 kijiko cha chai
Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Ukwaju ¼ kikombe
Namna Ya kutayarisha Na Kupika:
1. Changanya vitu vyote pamoja mroweke kuku kwa muda wa masaa
2. Mchome (broil) katika oveni au katika jiko la mkaa kama B.B.Q – mweke kando.
Sosi Ya Makaroni
Vitunguu maji viliyokatwa katwa 3
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Nyanya zilizosagwa 3
Nyanya kopo 1 kijiko cha supu
Pilipili manga 1 kijiko cha chai
Oregano 1 kijiko cha chai
Nanaa iliyokatwa katwa 2 msongo (bunch)
Chumvi kiasi
Mafuta ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha na Kupika
1. Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu maji hadi vigeuke rangi.
2. Tia thomu endelea kukaanga, tia nyanya, nyanya kopo, pilipili manga, oregano, chumvi endelea kukaanga.
3. Mwisho tia nana koroga sosi ikiwa tayari.
Makaroni Na Namna Ya Kupakua
1. Chemsha makoroni hadi yaive yachuje kwa kumwaga maji.
2. Pakuwa macaroni katika sahani au chombo na mwagia sosi juu yake kisha kuku, na tolea na saladi au mapilipili mboga.
No comments:
Post a Comment