
VIPIMO VYA SOSI
Vitungu vilivyokatwa 2 Kiasi
Thomu iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Nyanya ya kopo 1 kopo
Nyanya ziliyosagwa 3 Vikombe
Viungo vya Kiitali (Oregano,basil,thyme) 1 Kijiko cha supu
Chumvi Kiasi
Pilipili manga ya unga ½ Kijiko cha chai
Figili mwitu (celery) na pilipili mboga ½ Kikombe kila moja
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Katika sufuria kaanga vitungu kisha tia thomu.
2. Tia Nyanya, nyanya kopo na viungo vyote.
3. Tia pilipili mboga na figili mwitu na ukaange hadi zilainike.
4. Tayarisha kababu za nyama ya kusaga katika supu.
VIPIMO VYA KABABU
Nyama ya kusaga 1 LB (Ratili)
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Chumvi Kiasi
Pilipili mbichi iliyosagwa 1
Kotmiri iliyokatwa Kiasi
Garama Masala (bizari ya mchanganyiko) 1 Kijiko cha chai
Maji 2 Gilasi
Stock (Supu ya vidonge – Maggi cube) 1
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Changanya vipimo vyote katika bakuli isipokuwa maji na kidonge cha supu.
2. Fanya viduara vidogo vya mchanganyiko wa nyama viwe kama kababu, weka kando.
3. Chemsha maji kisha tia vidonge vya kababu vichemke
4. Tia kidonge cha supu (Stock)
5. Zikishawiva mimina sosi uliyotayarisha juu ya hii supu ya kababu.
6. Tayari kuliwa kwa kumwagiwa juu ya Spagetti.
SPAGETI
Chemsha Spagetti kiasi ya 300 gm, zikiwiva chuja maji zikiwa tayari kuliwa na sosi pamoja na zaytuni ukipenda.
No comments:
Post a Comment