
VIPIMO
Makaroni 500 gramu (gms)
Kamba wa barafu (frozen) saizi ya katikati 1000 gms
Malai (cream) 170 gms
Maziwa ya chai ya kopo 1/4 kikombe
Mafuta ya kukaangia 1/4 kikombe
Vitunguu vilivyokatwa vidogodogo 2
Karoti iliyokatwa ndogo ndogo 1
Pilipili kubwa kata ndogo ndogo 1
Figili mwitu (celery) kata ndogo ndogo 2 miche
Brokoli (brocoli) kata vipande vipande 1 msongo (bunch)
Nyanya iliyosagwa 1/2 kikombe
(au rojo ya nyanya (paste)
Pilipili mbuzi iliyokatwa ndogo ndogo 1
(ukipenda)
Mraba wa Maggi (maggi cubes)
ya kuku au nyama 2
Chumvi kiasi
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha supu.
NAMNA YA KUTAYARSIHA NA KUPIKA
1. Chemsha makaroni kwa chumvi na mafuta kidogo kwa kufuata maagizo yake katika karatasi. (usiyaivishe sana hadi yakavurugika)
2. Yakishawiva mwaaga maji kwa kuchuja.
3. Katika sufuria kubwa au karai, tia mafuta na kaanga vitunguu kidogo tu kama dakika 1 tu.
4. Tia pilipili mboga, karoti, pilipili mbuzi.
5. Mumunyia mraba ya Maggi (Maggi cubes)
6. Tia nyanya iliyosagwa au rojo ya nyanya na kaanga tena kidogo tu kama dakika moja.
7. Tia chumvi na pilipili manga.
8. Tia kamba na ukaange kidogo tu kwani huiva mara moja.
9. Mimina makaroni na changanya vizuri.
10. Tia brokoli, na figili mwitu (celery)
11. Malizia kwa kutia malai (cream) na maziwa na pika kwa dakika 2, ikiwa tayari kuliwa.


No comments:
Post a Comment