
Vipimo
Makaroni 500 gm
Nyama ya Kusaga 1 ratili
Vitunguu 2
Nyanya 3
Nyanya kopo (tomato paste) 3 vijiko vya supu
Brokoli 1 msongo (bunch)
Kitunguu Thomu [garlic] kilosagwa 1 kijiko cha chai
Pilipili manga 1 kijiko cha chai
Bizari ya oregano [Italian spice] 1 kijiko cha chai
Parsely (aina ya kotmiri) 2 misongo (bunches)
Sosi ya soya 2 vijiko cha supu
Mafuta ¼ kikombe cha chai
Karoti 2
Pilipili mboga 1
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha Makaroni kama inavyoeleza katika paketi, chuja maji weka kando.
- Katakata vitunguu, nyanya vipande vidogo vidogo weka kando
- Chambua brokoli weka kando.
- Katakata parsley ndogo ndogo (Chopped) weka kando.
- Weka mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kidogo tu.
- Tia nyama, kitunguu thomu, bizari zote endelea kukaanga hadi nyama iwive.
- Tia nyanya pamoja na nyanya kopo, tia brokoli, parsely, sosi ya soya endela kukaanga kidogo tu.
- Tia makoroni changanya vizuri.
- Pakuwa katika bakuli, mwagia karoti na pilipili mboga zilokatwa katwa ikiwa tayari.
No comments:
Post a Comment