Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 1 January 2014

Spageti Na Sosi Ya Nyama Ng'ombe Vipande



Vipimo




Spaghetti                                                                  500g

Maji                                                                         1lita na nusu

Chumvi                                                                    1 kijiko cha supu

Tomato ya kopo                                                       3 Vijiko vya supu

Tomato (fresh)                                                         3

Kitunguu maji                                                           1

Thomu iliyosagwa                                                     1 kijiko cha chai

Nyama  bila mifupa                                                   nusu kilo

Tangawizi mbichi ilyosagwa                                       1 kijiko cha supu

Mafuta                                                                     nusu kikombe cha chai


Namna ya kutayarisha sosi


  1. Nyama ikoshe na ukata vipande (size) upendayo,tia sufuriani.
  2. Itie tangawizi,chumvi nusu, na ipike kwa kuikausha moto wa chini bila kuongeza chochote paka itoe maji na kutowa harufu ya supu zima jiko.
  3. Kwenye sufuria nyengine katakata tomato, kitunguu,tia mafuta nusu mengine utatia kwenye spaghetti.
  4. Weka jikoni ongeza thomu,tomato ya kopo kijiko kimoja na pika kwa nusu saa.
  5. Saga mchanganyo wa mboga ulopika kwa machine ya kusagia (handy mixer); paka isagike kisha ongeza tena tomato ya kopo ilobakia usisage tena hapa.
  6. Rojo lile la mboga, mimina nyama changanya na rudisha kwenye jiko kwa moto wa chini na iache ipikike kwa muda wa dakika 45 – 50; Na sosi itakuwa tayari.

Spaghetti


  1. Sufuria ya nafasi tia maji weka katika jiko yaache mpaka yachemke kisha mimina spaghetti.Ziache mpaka ziive  toa moja ubonyeze ukiona imewiva ,chuja maji yote.
  2. Rudisha sufuriani kisha mimina chumvi na mafuta ulobakisha zipepete zichanganyike  mafuta vizuri.  Tayari kuliwa.

Kidokezo

Unaweza kukwaruza cheese kwenye spaghetti baada ya kupakuwa kama kwenye picha.

No comments:

Post a Comment