Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, 3 January 2014

Mchezaji wa Club ya Barcelona lionel messi aukwea mlima kilimanjaro kimya kimya

Mchezaji wa Club ya Barcelona, Lionel Andrés Messi mwishoni mwa mwaka 2013 alitua Tanzania kimya kimya kufanya tangazo la Turkish Airlines kwenye Mlima Kilimanjaro.
6812765_orig
Idea ya tangazo hilo ni kuwa Messi na mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Los Angeles Lakers, Kobe Bryant wanashindana kupiga picha bora zaidi aina ya selfie.

Tangazo linaanza kwa Messi kumtumia picha Kobe yake mwenyewe akiwa mbele ya kanisa la Saint Basil’s Cathedral mjini Moscow.
1316388_orig
Kobe naye anajibu mapigo kwa kwenda kwenye kuta maarufu za China (The Great Wall of China) na mashindano yanaendelea hadi kumfanya Messi aje kuchukua selfie kwenye mlima Kilimanjaro, huku maeneo yote hayo yakifikika na ndege za Turkish Airlines. Mwisho Messi anajipiga picha akiwa Sultanahmet Square mjini Istanbul, na kuja kugunduaa nyuma yake alikuwepo Kobe aliyetokea pia kwenye picha yake.
2130077_orig
8004664_orig
9903675_orig
Tazama tangazo lao hilo ambalo tangu liwekwe December 3 limeshaangalia kwa zaidi ya mara milioni 135.




No comments:

Post a Comment