Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, 3 January 2014

Sudan yaonya kuhusu mgogoro wa Sudan Kusini


Sudan yaonya kuhusu mgogoro wa Sudan Kusini
Kiongozi wa jimbo la Darfur la magharibi mwa Sudan, ameonya juu ya kushadidi mapigano huko nchini Sudan Kusini na kuwepo uwezekano wa kuzidiwa jimbo hilo na idadi ya makundi ya raia wanaoyakimbia makazi yao kutoka nchi hiyo jirani. At-Tijani Al-Sisi, Mkuu wa Harakati ya Uhuru
na Uadilifu nchini Sudan ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa jimbo la Darfur, amesema hayo na kuongeza kuwa, jimbo hilo kwa sasa halina uwezo wa kupokea wakimbizi zaidi kutoka Sudan Kusini. Al-Sisi amezitaka pande hasimu nchini Sudan Kusini kusimamisha mapigano na kuketi kwenye meza ya mazungumzo ili kuiokoa nchi yao. Kwa upande mwingine kiongozi huyo, ameyataka makundi yote ya waasi nchini Sudan kutounga mkono upande wowote katika mapigano yanayoendelea katika nchi jirani na badala yake yashiriki katika mchakato utakaosaidia kupatikana amani na usalama katika eneo hilo sambamba na kutekeleza makubaliano ya Doha, Qatar, kuhusiana na jimbo la Darfur. Hii ni katika hali ambayo wawakilishi wa pande hasimu katika mgogoro nchini Sudan Kusini, walianza kwa mara ya kwanza mazungumzo yao hapo jana huko mjini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kuutafutia utatuzi mgogoro wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
SOURCE : Iran Swahili

No comments:

Post a Comment