
Vipimo
Ndizi mbichi 10-12
Nyama ng’ombe 1 kilo moja
Kitunguu maji 2
Nyanya/tungule 2
Kitunguu thomu 7
Tangawizi mbichi 1 kipande
Ndimu 2 kamua
Chumvi kiasi
Mafuta 3 vijiko vya supu
Tui la nazi 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi.
2. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive.
3. Menya ndizi ukatekate
4. Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga.
5. Tia tangawizi na thomu ilobakia.
6. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake.
7. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
No comments:
Post a Comment