
Vipimo
Mpunga 4 vikombe
Nyama 1 kilo moja
Kitunguu maji 3
Mbatata/viazi 7 vidogodogo
Kitunguu thomu na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu
Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin 3 vijiko vya supu
Mdalasini 3 vipande
Hiliki 7 punje
Pilipili manga nzima 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Mafuta ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Osha mchele weka kando
2. Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo.
3. Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga.
4. Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi.
5. Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata.
6. Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari.
7. Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.


No comments:
Post a Comment