
Vipimo
Saladi la duara 1
Tango 1
Pilipili mboga jekundu ½
Pilipili mboga kijani ½
Pilipili mboga manjano ½
Karoti 1
Kitunguu cha zambarau (red onion) ½
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katakata saladi la duara lioshe, lichuje na lipange katikati kwenye sahani.
- Katakata matango slesi yapange kuzunguka sahani.
- Kuna (grate) karoti kisha mwagia juu ya saladi kisha katakata mapilipili mboga tupia tupia juu ya karoti.
- Kata kitunguu slesi kisha tupia tupia juu.
Kidokezo: Ukipenda changanya ndimu , mafuta ya alizeti (olive oil) na chumvi mwagia juu.
No comments:
Post a Comment