
Vipimo
Vipimo vya Wali:
Mchele 3 vikombe
*Maji ya kupikia 5 vikombe
*Kidonge cha supu 1
Samli 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Hiliki 3 chembe
Bay leaf 1
Vipimo Vya Kuku
Kidari (chicken breast) 1Kilo
Kitunguu 1
Tangawizi mbichi ½ kipande
Kitunguu thomu 7 chembe
Pilipili mbichi 3
Ndimu 2
Pilipilimanga 1 kijiko cha chai
Mdalasini ½ kijiko cha chai
Jira/Cummin ya unga 1 kijiko cha chai
Maji ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Wali:
- Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto.
- Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo.
- Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau.
*Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo.
* Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.
Kuku:
- Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi.
- Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku.
- Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri.
- Tia maji kiasi ¼ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)
No comments:
Post a Comment