Vipimo
Mchele wa Basmati /Pishori 4 vikombe
Kuku 1
Vitunguu 3
Nyanya/Tungule 2
Tangawizi mbichi ilosagwa 2 vijiko vya supu
Kitunguu thomu kilosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi nzima 3
Ndimu 2
Garama Masala/bizari mchanganyiko 1 kijiko cha supu
Haldi/tumeric/bizari manjano 1 kijiko cha chai
Pilipilu ya unga nyekundu 1 kijiko cha chai
Mtindi /yoghurt 3 vijiko vya supu
Mafuta ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele, roweka.
- Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli.
- Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu.
- Punguza mchanganyiko kidogo weka kando.
- Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi.
- Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive.
- Epua, weka kando.
- Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando.
- Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
- Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali.
- Tia kuku uchaganye vizuri.
- Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja.
- Punguza masala nusu yake weka kando.
- Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali.
- Funika upike katika oveni hadi uive.
- Changanya unapopakua katika sahani.
No comments:
Post a Comment