Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, 3 January 2014

Idadi ya wahanga wa mripuko wa jana Bairut yafikia 69



Idadi ya watu waliouawa na kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi la hapo jana jioni mjini Bairut Lebanon imepindukia watu 69. Waziri wa Afya wa Lebanon Ali Hassan Khalil
amesema kuwa, jumla ya watu 69 wameuawa na kujeruhiwa kufuatia shambulizi hilo lililotokea katika mji wa Harik katika viunga vya mji mkuu Bairut. Shambulio hilo la bomu la kutegwa ndani ya gari ulitokea jioni ya jana jirani na jengo la zamani la televisheni ya Al-Manar inayomilikiwa na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah. Aidha shambulio hilo la kigaidi, limepelekea uharibifu mkubwa wa majengo, magari na maduka ya jirani na sehemu palipotokea shambulio hilo la kigaidi. Vikosi vya Lebanon vinaendelea na upelelezi ili kuwapata wahusika. Siku ya Ijumaa iliyopita, watu wanane akiwemo Muhammad Shatah, waziri wa zamani wa fedha katika serikali ya Fouad Siniora waliuawa katika shambulio la kigaidi lililotoke mjini Bairut. Shambulio la jana limetokea katika hali ambayo kitengo cha masuala ya kiintelijensia na usalama cha jeshi la Lebanon kimetangaza kumkamata raia wa Saudi Arabia, Majid bin Muhammad al-Majid kiongozi wa kundi la kigaidi linalojiita Brigedi ya Abdullah Azzam lenye mfungamano na mtandao wa al-Qaeda mwenye uraia wa Saudia. Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naim Qassim, ametaka kuundwa haraka serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo. sambamba na kulaani shambulio la jana, amesema kuwa majibu bora kabisa ya kukabiliana na hali hiyo, ni kuundwa haraka serikali ya kitaifa nchini Lebanon.
SOURCE : Iran Swahili

No comments:

Post a Comment