Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, 3 January 2014

Saudia yataka kusafishwa jina lake kimataifa



Mrithi wa kiti cha ufalme nchini Saudia, amewataka mabalozi wa nchi hiyo katika nchi mbalimbali za duniani, kufanya juhudi ya kuimarisha uhusiano mwema na kusafisha jina la Saudia kimataifa. Salman bin Abdulaziz Al Saud ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Mrithi wa kiti cha ufalme na Naibu Waziri Mkuu wa Saudia ameyasema hayo alipokutana na baadhi ya
mabalozi wapya wa nchi hiyo katika nchi mbalimbali za dunia na kuashiria nafasi ya taifa hilo katika fikra za walio wengi na kusisitiza kuwa, hilo ni jukumu la mabalozi kusafisha jina la Saudia kimataifa. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, Saudia imekuwa ikikosolewa sana kimataifa kutokana na hatua yake ya kuyaunga mkono makundi ya kigaidi katika nchi mbalimbali kama vile Syria na Iraq. Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Saud bin Faisal bin Abdulaziz alimchagua Abdul-Rahman bin Ghirman Al Shahri, kuwa balozi wa nchi hiyo hapa nchini Iran. Hivi karibuni jarida la Veteran Today la Marekani liliandika kuwa, utawala wa kifalme wa Aal Saud nchini Saudia umekuwa ukiyasaidia kifedha makundi ya kigaidi na yale yenye kuwakufurisha Waislamu wengine katika eneo la Mashariki ya Kati. Aidha gazeti hilo limemtaja Bandar bin Sultan bin Abdulaziz, Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Saudi Arabia kuhusika na milipuko iliyotokea hivi karibuni nchini Russia na Lebanon.
SOURCE : Iran Swahili

No comments:

Post a Comment