Vipimo
Majani ya saladi (lettuce) ½ Msongo
Tango 1 kubwa
Nyanya 1
Parsley ¼ Kikombe
Nanaa (mint) Kiasi
Pilipili tamu la kijani 1
Pilipili kubwa jekundu tamu 1
Kitunguu cha majani kijani 1 Msongo
Majani ya methi ½ Kikombe
Mkate wa pita 1
Salsali (salad dressing)
Ndimu 2 Vijiko vya supu
Mafuta ya zaituuni ¼ Kikombe
Thomu iliyosagwa 1 chembe
Chumvi Kiasi
Pilipili manga ¼ Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha
- Katakata majani ya saladi na vipimo vyote isipikuwa mkate wa pita.
- Choma mkate wa pita katika oveni ibadilike rangi ya browni, kisha vunja vipande vipande.
- Changanya vyote vizuri katika bakuli la kiasi.
- Kisha changanya vitu vyote vya salsali pamoja.
- Karibu na kula mwagia dressing uchanganye vizuri ikiwa tayari kuliwa.


No comments:
Post a Comment