
Mahitajio
|
Utayarishaji
|
Kipimo
|
Parsley (aina ya kotmiri) Taz picha
|
osha, chuja maji katakata (chop)
|
4 misongo (bunches)
|
Nanaa (mint leaves)
|
“ “
|
1 msongo
|
Vitungu majani (spring onions)
|
katakata vidogodogo
|
7
|
Kitunguu maji
|
“ “
|
2
|
Tungule nyanya ya kawaida
|
“ “
|
3 kubwa
|
matango
|
“ “
|
3
|
burghur (ngano ilokobolewa) Tazama picha
|
¼ kikombe
| |
Limau
|
kamua
|
2
|
chumvi
|
kiasi
| |
mafuta ya zaytuni
|
1/3 kikombe
|
Namna Ya Kutayarisha
- Osha bulgur tia maji roweka muda robo saa, kisha ichuje maji na ukamue itoke maji yote.

- Katika bakuli weka vitu vyote isipokuwa limau, chumvi na mafuta ya zaytuni.
- Karibu na kupakua changanya bulgur, limau na mafuta ya zaytuni katika kibakuli kidogo kisha mwagia na changanya pamoja na vitu katika bakuli.
Kidokezo:
- Hakikisha umechuja maji majani na vitu vyote kwani Tabbulah hulegea mara moja. Na pia ni vyema kuchanganya vitu karibu na wakati wa kupakua
No comments:
Post a Comment