
Vipimo
Viazi 7 vya kiasi
Maharage machanga ya kijani (spring beans) 1 kikombe
Karoti 1 kikombe
Mahindi 1 kikombe
Njegere I kikombe
Mayonnaise 3 vijiko vya supu
Kitunguu Thomu 3 chembe
Chumvi kiasi
Pilipilimanga ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha viazi kiasi (visiive sana hadi kuvurugika). Kisha menya na kata vipande vidogovidogo, weka kando.
- Menya na kata karoti vipande vidogovidogo weka kando.
- Chemsha Maharage machanga (spring beans) mahindi na njegere. Karibu na kuwiva tia karoti. Maji ya kuchemshia yawe ya kiasi kidogo tu.
- Katika bakuli la kupakulia saladi, weka viazi, na karoti na njegere, maharage na mahindi uliyoyachemsha.
- Chuna au saga kitunguu thomu, changanya vizuri na mayonnaise, chumvi na pilipili manga. Kisha mimina katika bakuli pamoja na mchanganyiko wa viazi na mboga/maharage, ikiwa tayari.
KIDOKEZO:
Karoti na aina za njegere, maharage na mahindi zinapatikana tayari madukani katika freezer, na hazihitaji kuchemshwa sana.
No comments:
Post a Comment